TANGAZO
Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar(CGCLA) inawatangazia wadau wote wanaojishughulisha na utumiaji, uingizaji, utoaji pamoja na usambazaji wa kemikali na bidhaa zitokanazo na kemikali wanatakiwa kufika ofisi kuu Maruhubi kwa ajili ya kujisajili au kufika ofisi ndogo zilizopo Bandari kuu ya Malindi, Baraza la leseni Malindi na ofisi ndogo iliyopo Madungu Chakechake Pemba.
Aidha, Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar inawataka watoa huduma wote wa kupiga dawa za kuulia wadudu(fumigation) kuwa wanasajiliwa pamoja na kemikali zao kwani kutoa huduma hiyo bila ya kusajiliwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni kwenda kinyume na sharia namba 10 ya mwaka 2011 na kanuni ya kemikali ya mwaka 2014
Kwa tangazo hili Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inawata wadau wote kufika ofini hapo si zaidi ya tarehe 30/11/2023 muda na saa za kazi,
Ahsante
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA UHUSIANO
WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI