Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(CGCLA) inapenda kuwatangazia huduma ya Mafunzo ya uchukuaji wa sampuli za vinasaba (DNA)
Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inawatangazia Mafunzo ya Uchukuaji wa Sampuli za Vinasaba (DNA) Kwa Askari Polisi na Watendaji wa Afya (Medical Practitioners) yatakayofanyika tarehe 02 Disemba Hadi tarehe 06 Disemba 2024 ofisini kwao Maruhubi.
Fomu ya Maombi inapatikana katika tovuti ya Taasisi www.cgcla.go.tz Mwisho wa Maombi haya ni tarehe 25 Novemba 2024.Bonyeza hapa kuthibitisha ushiriki wako
Mafunzo haya yatafanyika Kwa gharama ya Tsh.390,000(02 Disemba Hadi tarehe 04 Disemba 2024)
Kwa Watendaji wa Afya na Tsh. 260,000 (05 Disemba Hadi tarehe 06 Disemba 2024) Kwa Askari wa Jeshi la Polisi.
Kwa mawasiliano zaidi piga Simu Namba 0774 774 674 au 0 713 704 016.
N.B WATENDAJI WA VITUO VYA MKONO KWA MKONO WANASHAURIWA KUSHIRIKI ZAIDI