Email: info@cgcla.go.tz
Left Image

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST LABORATORY AGENCY

Right Image
Home /News

Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar yazindua Mfumo wa usimamizi wa kemikali.

Zanzibar, Tarehe 30/07/2025
  • Akizindua mfumo huo tarehe 30-7-2025 katika Hoteli ya Madinat Al Bahr iliyopo Mbweni Mjini Zanzibar Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said amesema lazima kemikali zifanyiwe udhibiti ili kuepusha madhara pamoja mustakabali wa Nchi kukaa sawa katika suala la afya jamii na kuzichunga ili kuzuia matumizi yasiyo na uhalali..
  • Mhandisi alieleza kuwa,tumaini letu mfumo huo utapunguza ajali za kemikali, Wadau watawajibika ipasavyo,utarahisha ukaguzi na utafiti wa uchumi wa Nchi kuwa endelevu kupitia kazi zinazofanywa na Mkemia wa Serikali, utasaidia hatua ya kihistoria ya kulinda afya ya Wananchi na kuhifadhi mazingira ya kizazi cha sasa na baadae pamoja na kudhibiti kemikali kwa usalama wa taifa..
  • Aidha, alipongeza juhudi zilizofanywa na Wizara ya Afya, Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Wadau wote walishiriki kuandaa na kufanisha uzinduzi wa mfumo huo.
Mhadisi Zena
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said akizindua mfumo wa Udhitibi Kemikali Zanzibar ZCMP- katika Hoteli ya Madinat Al Bahr iliyopo Mbweni Mjini Zanzibar

  • Kwa upande wake, Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Farid Mzee Mpatani amesema, taasisi imepiga hatua kubwa za uchunguzi wa Maabara, hivyo, tukio la uzinduzi wa mfumo huo utasaidia kuimarisha maendeleo kutokana na kuongezeka na matumizi ya kemikali.
  • Mkemia Mkuu,alifafanua na kueleza kuwa, mfumo umejumuisha usajili wa Wadau wa kemikali zote, taarifa za usalama,ufuatiliaji wa usalama na ukumbusho wa kemikali.
  • Mbali na hayo, Dtk.Mpatani alisema taasisi inatarajia mfumo huo utasaidia usimamizi wa mfumo wa usajili wa kemikali, kupata data sahihi na kudhibiti matumizi mabaya ya kemikali katika athari za kimazingira na kiafya.
Mkemia Mkuu Dkt. Farid Mzee Mpatani
Mkemia Mkuu Dkt. Farid Mzee Mpatani

  • Sambamba na hayo, Mkurugenzi Wizara ya Afya Dkt.Amour amesisitiza kuwa, mfumo utaimarisha usalama wa matumizi ya kemikali Zanzibar..
  • Hivyo, Serikali imeona haya ya kuanzia mfumo huo kupitia Taasisi ya Mkemia Mkuu ili kuweza kwenda Sambamba na utekelezaji wa vipao mbele vyao vya kuanzisha mfumo wa kidigitali lengo ni kupunguza ajali za kemikali, dharura za kemikali, kupunguza gharama za utoaji wa huduma kwa Wadau na kusaidia kuendeleza mfumo wa viwanda na kuhifadhi mazingira. .
Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza kwa waandishi wa habari
Mkurugenzi Wizara ya Afya Dkt.Amour

  • Mkurugenzi wa Kemikali Ndugu Ussi Makame Kombo, alipongeza jitihada zilizochukuliwa na Serikali kwa kufanikisha mfumo na kuwataka wafanyakazi kuhakikisha wanatelekeza majukumu yao ya utoaji wa huduma kupitia mfumo huo kwa wakati kwa maendeleo ya taasisi na taifa kwa ujumla..
  • Washiriki wa uzinduzi wa mfumo huo, walipongeza jitihada zilizochukuliwa na Serikali za kufanikisha uzinduzi wa mfumo wa usimamizi wa kemikali na kuahidi kuleta mabadiliko chanya yatayoleta tija katika taifa leta. .
Mr. Ussi Makame Kombo
Mr Ussi Makame Kombo